RAIS Dk.John Magufuli amewaongoza viongozi wa ngazi mbalimbali pamoja na Watanzania kupokea ndege mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 262 aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ambayo imetua katika ardhi ya Tanzania saa 11.25 jioni.
Ndege hiyo kabla ya kutua ilichukua dakika kadhaa ikionekana katika anga la Tanzania huku Rais Magufuli na Watanzania kwa ujumla wakiishangilia wakati inashuka.
Mbali na Rais Magufuli pia alikuwepo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan , Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali.
Baada ya ndege hiyo kutua ilipata heshima ya kumwagiwa maji kama ishara ya kuipokea rasmi.
Ndege hiyo ambayo ni kubwa na ya kisasa baada ya kupata heshima ya kumwagiwa maji kama ishara ya kuikaribisha ilikwenda eneo maalumu ambalo Rais amewaongoza Watanzania wengine kuipokea.
Baada ya ndege hiyo kusimama rasmi ulifunguliwa mlango ili waliokuja nayo washuke ambapo mlango ulifunguliwa saa 11:38 ambapo marubani walioleta ndege walikuwa wa kwanza kushuka huku wakipunga mkono.
Upload by KidaniStars channel id: UCpg9aDs4Brj4atWcoHYPtFQ , jaNwWXZizE0.
0 Comments